Skip to main content

MAFUNZO YA UFUNDISHAJI LUGHA

USULI

Ufundishaji lugha ya kigeni ni taaluma mtambuka ambayo imekuwa ikijadiliwa na wataalamu mbalimbali karibu kila siku. Suala la mbinu za ufundishaji, utambuzi wa viwango vya lugha na uhusishaji utamaduni katika darasa la lugha ya kigeni yamepewa kipaumbe katika mijadala hii ili kumfanya mwalimu wa lugha ya kigeni kuleta matokeo mazuri kwa wajifunzaji. Kutokana na umuhimu wa taaluma hii, mafunzo mahususi yameandaliwa ili kuwezesha wataalamu wa ufundishaji lugha na waratibu kuweza kuandaa na kufundisha Kiswahili kwa wageni kwa ufanisi.

MADA

 • Dhana ya ufundishaji lugha ya kigeni
 • Mikabala ya ufundishaji lugha ya kigeni
 • Utambuzi wa viwango vya lugha kwa wajifunzaji
 • Uandaaji andalio la somo
 • Uandaaji zana za kufundishia
 • Mbinu za ufundishaji kuzingatia mkabala wa kimawasiliano
 • Umahiri wa kimawasiliano na tamaduni mchangayiko
 • Namna ya kujitangaza na kupata wajifunzaji

WALENGWA WA MAFUNZO

 • Waratibu na walimu wa programu za ufundishaji wa Kiswahili kwa wageni
 • Wataalamu wa uandaaji wa mitaala
 • Walimu wa lugha nyingine za kigeni (Kifaransa, kijerumani, kichina na n.k)

 

 

MAHITAJI YA MSHIRIKI

 • Mshiriki anapaswa kushiriki mafunzo akiwa na zana zifuatazo:
 • Kompyuta (laptop) yenye kamera au kamera ya nje (webcam) na kasi ya ram angalau 4 GB na kuendelea;
 • Headphones; na USB Drive
 

ADA

Ada ya Ushiriki - TZS 250,000/=

 

JINSI YA KULIPA

 • Jina la Benki: CRDB
 • Jina la akaunti: MSTCDC
 • Namba ya akaunti: 0150 4064 25901
 • Maelezo: SWAHILI TOT

 

THIBITISHA USHIRIKI

Mwl Said Omar: omars@mstcdc.or.tz / +255 713 727 806 au +255 742 727 874

In the words of others

GET OPPORTUNITIES AND STORIES DIRECTLY IN YOUR INBOX

Subscribe now